Je, unasumbuliwa na tatizo la Tezidume (Prostate Enlargement)?
Kama umekuwa ukikabiliwa na changamoto zifuatazo, basi makala hii ni muhimu sana kwako:
- Kuchoka kutumia dawa za tezidume kila siku bila kupata nafuu ya kudumu
- Hofu ya matibabu yanayoweza kuathiri nguvu za kiume (erection)
- Wasiwasi wa kupoteza uwezo wa kutoa manii au kupata watoto
- Kutotaka kufanyiwa upasuaji
- Kutamani tiba ya mara moja itakayorejesha mkojo wako kuwa wa kawaida
- Kutaka kurudi kwenye majukumu ya kila siku ndani ya muda mfupi
Sasa suluhisho limepatikana.
REZUM WATER VAPOR THERAPY NI NINI?
REZUM Water Vapor Therapy ni tiba ya kisasa kabisa ya matibabu ya tezidume (Benign Prostatic Hyperplasia – BPH) inayotumia mvuke maalum wa maji (steam) kuondoa seli za tezidume zilizovimba na kusababisha kuziba kwa njia ya mkojo.
Mvuke huu huathiri tu seli zilizoathirika bila kuharibu mishipa muhimu inayohusika na:
- Kusimama kwa uume
- Utoaji wa manii
- Uwezo wa kupata watoto
FAIDA ZA REZUM WATER VAPOR THERAPY
✔ Hakuna upasuaji
✔ Hakuna matumizi ya dawa kwa muda mrefu
✔ Haitoi athari kwenye nguvu za kiume
✔ Haitoi athari kwenye uzazi
✔ Huchukua chini ya dakika 30
✔ Huhitaji kulazwa hospitalini
✔ Unarejea nyumbani siku hiyo hiyo
✔ Unarudi kwenye shughuli zako za kawaida kwa haraka
HUDUMA HII INAPATIKANA WAPI?
Hospitali ya KCMC, kwa kushirikiana na Shyadri Hospital – Pune, India, chini ya uratibu wa Tanlink Medical Tourism Agency, inawaletea Watanzania huduma hii ya kibingwa kupitia:
🏥 KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA TEZIDUME
📍 Hospitali ya KCMC – Moshi, Kilimanjaro
📅 Tarehe: 26 – 31 Januari 2026
Hii ni fursa adimu ya kupata tiba ya kiwango cha kimataifa hapa hapa nchini.
JINSI YA KUJISAJILI
Ili kushiriki katika kambi hii ya matibabu, unapaswa kujisaajili kabla ya tarehe 26 Januari 2026 kupitia njia zifuatazo:
- 📌 Kufika Hospitali ya KCMC – Moshi
- 📌 Kufika Ofisi za Tanlink Medical Tourism Agency,
Posta Mpya, Haidery Plaza, Ghorofa ya Pili – Dar es Salaam - 📞 Kupiga simu:
- 0744 735 770
- 0711 989 838

