Je, unasumbuliwa na maumivu ya mgongo kwa muda mrefu?
Maumivu ya mgongo ni tatizo linalowaathiri watu wengi na mara nyingi huathiri ubora wa maisha, utendaji kazini na ustawi wa mwili kwa ujumla. Ikiwa unapitia mojawapo ya changamoto zifuatazo, makala hii ni muhimu sana kwako:
- Maumivu ya mgongo ya muda mrefu na umechoka kutumia dawa za maumivu kila siku
- Maumivu yanayoanzia mgongoni na kushuka hadi kwenye mapaja au miguu
- Hofu ya kutumia dawa za maumivu kwa muda mrefu kutokana na madhara kwenye figo
- Unahitaji kutuliza maumivu haraka ukiwa unajiandaa kwa upasuaji
- Unashindwa kufanya tiba-mazoezi (physiotherapy) kwa sababu maumivu ni makali
- Maumivu yanaongezeka unapofanya physiotherapy
- Umeambiwa na daktari kuwa diski za mgongo zimechakaa
- Umeambiwa kuwa diski ya mgongo inakandamiza mishipa ya fahamu
Sasa kuna suluhisho la kisasa, salama na lenye ufanisi.
EPIDURAL STEROID INJECTION (ESI) NI NINI?
Epidural Steroid Injection (ESI) ni tiba ya kisasa ya kitabibu inayotumika kutuliza na kupunguza maumivu ya mgongo yanayosababishwa na:
- Disc bulge au disc herniation
- Kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu
- Degenerative disc disease
- Sciatica
- Maumivu ya mgongo ya muda mrefu
Tiba hii hutumia dawa maalum ya steroid inayodungwa moja kwa moja kwenye eneo la mgongo (epidural space) lenye uvimbe au msongo wa mishipa ya fahamu ili kupunguza uvimbe na maumivu.
FAIDA ZA EPIDURAL STEROID INJECTION
✔ Hupunguza maumivu kwa haraka
✔ Hupunguza au kuondoa hitaji la kutumia dawa za maumivu kila siku
✔ Huwezesha mgonjwa kuanza au kuendelea na physiotherapy bila maumivu makali
✔ Husaidia kuahirisha au kuepuka upasuaji kwa baadhi ya wagonjwa
✔ Hutolewa ndani ya dakika 30
✔ Hakuhitaji kulazwa hospitalini
✔ Mgonjwa huruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo
NANI HUTOA HUDUMA HII?
Huduma ya Epidural Steroid Injection hutolewa na madaktari bingwa wa magonjwa ya mgongo na mishipa ya fahamu, kwa kutumia vifaa vya kisasa na kufuata viwango vya juu vya usalama wa kimataifa.
HUDUMA HII INAPATIKANA WAPI NA LINI?
Hospitali ya KCMC, kwa kushirikiana na Sahyadri Hospital – Pune, India, chini ya uratibu wa Tanlink Medical Tourism Agency, inawaletea huduma hii kupitia:
🏥 KAMBI YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BOBEZI
📍 Hospitali ya KCMC – Moshi, Kilimanjaro
📅 Tarehe: 26 – 31 Januari 2026
Kambi hii itahusisha madaktari bingwa na bobezi kutoka India na Tanzania, ikilenga kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa maumivu ya mgongo.
JINSI YA KUJISAJILI
Ili kushiriki kwenye kambi hii na kupata huduma ya Epidural Steroid Injection, unapaswa kujisajili kabla ya tarehe 26 Januari 2026 kupitia:
- 📌 Hospitali ya KCMC – Moshi
- 📌 Ofisi za Tanlink Medical Tourism Agency
Posta Mpya, Haidery Plaza, Ghorofa ya Pili – Dar es Salaam - 📞 Simu:
- 0744 735 770
- 0711 989 838

