ZIFAHAMU HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA KWENYE KAMBI YA MATIBABU YA KIBINGWA KWA MAGONJWA YA MACHO DAR

Tanlink Medical Tourism Agency kwa kushirikiana na International Eye Hospital ya Dar es Salaam na Andalusia Hospital kutoka Cairo, Misri, wanakukaribisha kushiriki katika kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya macho.

📅 Tarehe: 29 Juni – 03 Julai 2026
📍 Mahali: International Eye Hospital, Kinondoni – Morocco, Dar es Salaam

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:

✅ Kuonana na madaktari bingwa na wabobezi wa macho kutoka Misri na Tanzania kwa ushauri wa kina (Consultation)

✅ Kufanyiwa uchunguzi wa afya ya macho kwa ujumla

✅ Vipimo na uchunguzi wa kina wa matatizo ya macho kwa watoto na watu wazima

✅ Matibabu ya kibingwa na ubobezi kwa kutumia dawa na upasuaji wa kisasa wa macho

✅ Elimu kuhusu magonjwa ya macho na namna ya kujikinga nayo

Usikose nafasi hii ya kupata huduma za kibingwa kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu wa kimataifa.

📝 Jisajili mapema katika International Eye Hospital au ofisi za Tanlink Medical Tourism Agency, Haidery Plaza, Ghorofa ya Pili, Posta Mpya, Dar es Salaam.

📞 Kwa maelezo zaidi:
0760 003 535
0654 725 770

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *