Tanlink Medical Tourism Agency Yapokea Ugeni Kutoka MOI

Tanlink Medical Tourism Agency leo imepata heshima ya kupokea ugeni kutoka Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) katika ziara ya kikazi iliyolenga kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili.

Ziara hiyo imeonesha dhamira ya pamoja ya kuendelea kushirikiana katika kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kupitia ushirikiano unaojenga thamani na kuongeza fursa za kuwafikia wagonjwa kwa urahisi zaidi.

Tanlink Medical Tourism Agency inaendelea kuthamini ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kama sehemu ya jitihada za kuboresha huduma na kuchangia maendeleo ya sekta ya afya nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *