HUDUMA YA KUSIMAMIA USAFIRISHAJI WA WAGONJWA

Je, umewahi kujiuliza ni jinsi gani mgonjwa anaweza kusafirishwa kwa usalama kutoka eneo moja kwenda lingine anapohitaji matibabu maalum?

Tanlink Medical Tourism Agency tumebobea katika huduma za kusafirisha wagonjwa (patient transfer services) kwa usalama, weledi na uangalizi wa karibu. Tunahakikisha mgonjwa anafika hospitalini, anapata matibabu anayohitaji na hata kurudi nyumbani bila changamoto.

Huduma hii ni muhimu sana kwa wagonjwa ambao:

  • Hawawezi kusimama au kutembea
  • Hawawezi kukaa kwa muda mrefu
  • Wanahitaji oksijeni muda wote (oxygen-dependent patients)
  • Wanahitaji uangalizi maalum wakati wa safari
  • Wanahitaji msaada wa kuhamishwa kutoka nyumbani kwenda hospitali au kwenda nchi nyingine kwa matibabu (medical travel)

Tunachokufanyia Katika Usafirishaji wa Wagonjwa

Tunaratibu kila hatua ya safari ya mgonjwa ili kuhakikisha usalama, faraja na muda unatumika vizuri. Huduma zetu zinajumuisha:

1. Usafiri kutoka Nyumbani hadi Uwanja wa Ndege (Home to Airport Transfer)

Tunamsaidia mgonjwa kuondoka nyumbani kwa kutumia gari la wagonjwa (ambulance) au gari maalum kulingana na hali yake ya kiafya. Wafanyakazi wetu waliofunzwa wanahakikisha mgonjwa anachukuliwa kwa uangalifu na kufikishwa kwa wakati.

2. Msaada wa Kumwingiza Mgonjwa Kwenye Ndege (Airport Assistance)

Tunakusimamia taratibu zote za uwanja wa ndege, ikiwa ni pamoja na:

  • Kumsogeza mgonjwa kutoka kwenye ambulance hadi ndani ya jengo la Airport
  • Kumsaidia wakati wa ukaguzi (check-in)
  • Kumuweka kwenye viti maalum (wheelchair assistance or stretcher arrangement)
  • Kuratibu na mashirika ya ndege kwa ajili ya ruhusa za kiafya (medical clearance)

3. Kupokea Mgonjwa Ndege Itakaposhuka (Arrival Coordination)

Tunashirikiana na timu katika nchi au mji anakokwenda mgonjwa ili kuhakikisha anapokelewa kwa:

  • Ambulance iliyoandaliwa
  • Wahudumu wa afya walio tayari kuendelea na uangalizi
  • Usafiri wa moja kwa moja kwenda hospitali (Airport to Hospital Transfer)

4. Kusaidia Mgonjwa Kwenye Safari Zote za Ndani ya Matibabu

Kwa kipindi chote cha matibabu, Tanlink Medical Tourism Agency tunasimamia:

  • Kufika hospitali kwa miadi (appointments)
  • Majaribio na vipimo (medical tests)
  • Movement zote muhimu hadi kumaliza matibabu

Tunakuwepo kuhakikisha mgonjwa hawahangaiki na usafiri, malipo, au huduma za ufuatiliaji.


Kwa Nini Uchague Tanlink Medical Tourism Agency?

  • Uzoefu wa miaka kadhaa katika medical transportation
  • Huduma salama na zenye uangalizi wa kitaalamu
  • Timu ya wahudumu waliobobea katika kushughulikia wagonjwa wenye uhitaji maalum
  • Uunganisho na hospitali ndani na nje ya Tanzania
  • Huduma za haraka, za kuaminika na zinazojali hali ya mgonjwa

Wasiliana Nasi

Iwapo una mgonjwa katika yoyote ya hali hizi, usisite kuwasiliana nasi kwa usaidizi wa haraka.

📍 Ofisi: Posta Mpya, Mtaa wa India na Kisutu, Jengo la Haidery Plaza, Ghorofa ya Pili – Dar es Salaam
📞 Simu:
• 0786 33 34 64
• 0763 36 34 64

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *