Kitaalamu, mbegu za kiume au sperm cells ndizo
zinazobeba vinasaba vya mwanaume na
kuungana na yai la mwanamke ili kuunda mimba.
Uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke
mimba unategemea ubora na wingi wa mbegu
hizi pamoja na nguvu zake za kiume. – Kitaalamu, tunapochunguza mbegu za kiume
tunazingatia mambo manne makuu:
1) Volume;
Kiasi cha shahawa. Kwasababu kwa kawaida
mwanaume anatakiwa kutoa angalau 1.5ml
kwa mzunguuko mmoja,Kiasi kidogo sana chini
ya hapo mara nyingi huashiria kasoro ya tezi za
uzazi au kuziba kwa mirija ya mbegu.
2) Count (idadi);
Mbegu zinapaswa kuwa angalau milioni 15 kwa
millilita moja ya shahawa. Chini ya hapo tunaita
oligospermia na mbegu Kukosekana kabisa
huitwa azoospermia.
3) Motility (uogeleaji);
Zaidi ya asilimia 40 ya mbegu zinatakiwa
kuogelea vizuri. Mbegu zisizo na nguvu au
zisizo sogea kabisa haziwezi kufika kwenye
yai.
4) Morphology (umbo la mbegu);
Angalau asilimia 4–5 zinatakiwa kuwa na umbo
sahihi, kwa sababu mbegu zenye kichwa au
mkia usio wa kawaida haziwezi kupenya yai.
5) Viability (uhai);
Asilimia kubwa ya mbegu zinapaswa kuwa hai,
siyo zilizokufa.”
Changamoto hizi hutokana na mambo mengi;
i) Homoni;
Kushuka kwa testosterone au matatizo ya
pituitary.
ii) Afya;
Varicocele (mishipa ya korodani kupanuka, au
kujikunja kunja na kutengeneza vijivimbe vidogo
vidogo ndani ya korodani, maambukizi, au
saratani ya korodani.
iii) Mazingira na tabia;
Uvutaji sigara, pombe, dawa za kulevya, lishe
duni, au joto la mara kwa mara kwenye korodani.
iv) Vinasaba;
Baadhi ya wanaume huzaliwa na kasoro
zinazozuia mbegu kutengenezwa vizuri.
Msikilizaji, kuna jambo la muhimu kulifahamu.
Upungufu wa mbegu za kiume sio sawa moja kwa
moja na upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume
anaweza kuwa na nguvu za kufanya tendo la ndoa,
lakini mbegu zake zikawa chache au dhaifu. Vilevile,
mwanaume anaweza kuwa na idadi ya kutosha ya
mbegu lakini akawa na tatizo la kusimamisha uume
kwa muda wa kutosha. Hata hivyo, mambo haya
mawili mara nyingi huingiliana: kwa mfano, homoni
ndogo ya testosterone inaweza kusababisha mbegu
chache na pia kupunguza nguvu za kiume.
Kwa kawaida, mwanaume mwenye changamoto za
mbegu hana dalili za moja kwa moja. Mara nyingi
hujulikana kupitia kushindwa kumpa mwanamke
mimba baada ya miezi 12 ya kujaribu bila kinga.
Lakini ishara zinazoweza kuambatana ni pamoja
na;
i)Kupungua kwa nguvu za kiume
ii)Uwezo mdogo wakukabiriana na tendo la ndoa
iii)Kukosa kabisa matamanio ya tendo la ndoa
iv) Maumivu au uvimbe kwenye korodani.
v) Kupungua kwa nywele za mwili au mabadiliko
ya matiti kwa wanaume, ishara ya homoni
kupungua.
Changamoto za mbegu hupelekea tatizo la uzazi
kwa wanaume, ambalo linaweza kuathiri ndoa,
familia na hata kisaikolojia ya mwanaume. Kwa
baadhi ya watu, chanzo cha tatizo linaweza
kufichua ugonjwa mkubwa zaidi, ikiwemo saratani
ya korodani au matatizo ya homoni.
WASILIANA NA TANLINK MEDICAL TOURISM AGENCY KWA MSAADA WA MATIBABU 0786 333 464 AU 0763 363 464

