Katika jitihada za kuikuza sekta ya Utalii Tiba nchini Tanzania, Tanlink Medical Tourism Agency kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliandaa tukio maalum lijulikanalo kama Good Doctors Dinner Talk – Kilimanjaro.
Huu ulikuwa ni usiku wa kitaalamu uliowakutanisha madaktari bingwa, mabobezi, madaktari wa kada mbalimbali, wataalamu wa lishe, physiotherapists na psychologists kwa lengo la kujadili namna teknolojia inavyoweza kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa ndani na nje ya Tanzania.
Katika usiku huu wa kitaalamu, washiriki walipata fursa ya kujadili mada muhimu ikiwemo:
1. Namna Teknolojia Inavyoweza Kurahisisha Huduma za Afya
Madaktari walikubaliana kuwa matumizi ya telemedicine, AI/automation, EMR systems na digital referrals yana nafasi kubwa ya kupunguza muda, gharama na usumbufu kwa wagonjwa.
2. Ushirikiano Kati ya Sekta Binafsi na Hospitali za Rufaa
Wadau walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano ili kuboresha ubora wa huduma, kuongeza wataalamu na kupanua upatikanaji wa matibabu ya kibingwa.
Nani Walihudhuria?
Tukio hili liliwahusisha:
- Madaktari Mabobezi (Super Specialists)
- Madaktari Bingwa (Specialists)
- Residents na General Practitioners
- Nutritionists, Physiotherapists & Psychologists
- Wawakilishi wa hospitali, sekta binafsi na wadau wa utalii tiba
Uwepo wao uliufanya mjadala kuwa wa kina na wenye kutoa mwelekeo mpya katika sekta ya afya.
Hitimisho
Tukio la Good Doctors Dinner Talk – Kilimanjaro limefungua njia mpya ya ushirikiano kati ya wataalamu wa afya na sekta ya utalii tiba.
Tanlink Medical Tourism Agency inasalia na dhamira ya kuhakikisha Tanzania inakuwa moja ya nchi vinara katika utoaji wa huduma za afya za ubora wa kimataifa.


