Kuvunjika kwa mfupa ni tatizo linaloweza kumpata mtu yeyote—iwe ni kutokana na ajali, michezoni au shughuli za kila siku. Bila matibabu sahihi na ya haraka, mgonjwa anaweza kupata adhari za papo kwa hapo, za muda mfupi au za muda mrefu ambazo zinaweza kusababisha ulemavu au hata kupoteza maisha.
🔴 Adhari za papo kwa hapo:
• Kuumia kwa misuli, mishipa ya fahamu, viungo au kuvuja damu
• Mbavu kuvunjika na kutoboa mapafu
🟠 Adhari za muda mfupi:
• Kupoteza damu nyingi na shock
• Kushindwa kupumua (ARDS)
• Mafuta kutoka mfupani kuingia kwenye damu (fat embolism)
• Kuziba mishipa ya damu kuelekea mapafu (pulmonary embolism)
🟢 Adhari za muda mrefu:
• Mfupa kuchelewa kuunga au kutokuunga kabisa
• Mfupa kuunga vibaya / kuwa mfupi
• Jointi kukakamaa
• Mfupa kuharibika au kuoza (kidonda ndugu)
• Misuli kubadilika na kuwa mfupa
👉 Matibabu ya haraka hupunguza hatari hizi na kumuepusha mgonjwa na ulemavu wa kudumu.
Kwa huduma za matibabu ya mifupa na changamoto nyingine za afya, tembelea ofisi yetu Haidery Plaza, ghorofa ya pili – Posta Mpya, Dar es Salaam.
📞 0786 333 464 | 0763 363 464


