Fahamu Dalili za Mawe Kwenye Mfumo wa Nyongo

Mawe kwenye nyongo hujengeka kimya kimya na taratibu sana tena  bila ya dalili yoyote ya mapema. Lakini kadiri mawe hayo yanavyoongezeka ukubwa au idadi basi dalili huanza kutokea na mgonjwa huweza kuonyesha dalili zifuatazo

1.Dalili ya kwanza — ambayo hutokea mara nyingi— ni maumivu makali upande wa juu kulia wa tumbo. Maumivu haya yanayoweza kuanza ghafla, kuongezeka kwa kasi, na kudumu dakika kadhaa hadi masaa kadhaa. Wakati mwingine, maumivu haya huenda hadi mgongoni au kwenye bega la kulia.”

2. Dalili ya pili ni Maumivu ya tumbo hasa Baada ya Kula Vyakula Vya Mafuta. Hii ni kwa sababu ya kusisimuliwa kwa nyongo kutoa enzymes za vyakula vya mafuta kunakosababishwa na vyakul vya mafuta ambavyo mtu amekula. Hii ni ishara nyingine muhimu

3. Dalili ya tatu ni Kutapika na Kichefuchefu cha mara kwa mara, hasa kinachoambatana na maumivu ya upande wa kulia wa tumbo. Hii ni dalili inayojirudia kwa watu wengi wenye mawe kwenye nyongo.”

4. Dalili ya nne ni  Kuhisi tumbo kujaa haraka, kuongezeka kwa gesi au kiungulia baada ya kula . Hii nayo ni inaweza kuwa dalili ya njia ya nyongo iliyozibwa na jiwe.”

5.Dalili ya tano ni Homa na Kutetemeka. Hii mara nyingi hutokea ikiwa mawe yamesababisha maambukizi ya bacteria katika mfuko wa nyongo, mwili unaweza kuonyesha homa, baridi kali au kutetemeka. Hii ni dalili inayohitaji matibabu ya haraka.

6. Dalili ya tano ni rangi ya Njano  katika Ngozi au macho. Dalili hii inaashiria kuwa jiwe limeziba njia za nyongo. Ni ishara hatari inayohitaji uangalizi wa kitabibu wa haraka.”

“Kwa hivyo, usipuuzie maumivu ya upande wa kulia wa tumbo, kichefuchefu kisichoeleweka, au kujaa kwa tumbo baada ya chakula. Mara nyingi, mwili huongea… ni jukumu letu kumsikiliza.”

“Chukua hatua mapema. Pata vipimo. Linda afya yako “

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *